APPLICATION FORM - DOC 2
Document Sample


YOUTH TO YOUTH FUND.
YOUTH TO YOUTH FUND.
MAELEZO KWA KISWAHILI
TAFSIRI YA “INFORMATION NOTE” UK. 2
TAFSIRI YA “SHORT PROPOSAL FORM” UK . 8
INNOVATE.
INNOVATE.
ACTIVATE.
ACTIVATE.
APPLY.
APPLY.
TANZANIA
Youth Entrepeneurship Facility
2 0 1 0
www.ilo.org/yen 1
1. NI NINI KIIKINI NA MALENGO YA MFUKO WA RUZUKU WA VIJANA-“
YOUTH-TO-YOUTH FUND”
Utangulizi The Youth Entrepreneurship Facility ni mradi wa kimaendeleo uaolenga
kuendeleza ujasiria mali kwa vijana, ni mradi unaoendeshwa na shirika la
kazi duniani (ILO) kwa kushirikiana na mtandao wa ajira kwa vijana, kwa
ufadhili wa kamisheni ya maendeleo ya Africa chini ya Mpango wa
maendeleo wa serikali ya Denmark.
Lengo kuu la mradi huu ni kukuza ajira kwa vijana kupitia uendelezaji
ujasiriamali endelevu kwa vijana wa Afrika Mashariki yaani vijana wa
kitanzania, Kenya na Uganda. Mradi huu utajenga ujasirilia mali kwa vijana
kwa kushirikiana na wadau mbalimbali na hasa vijana kupitia shughuli na
mikakati mbalimbali ikiwemo, kampeni za kuhamasisha utamaduni wa
ujasiriamali, kuendeleza mitaala na kujenga stadi za ufundishaji wa elimu
ya ujasiriamali mashuleni, kujenga mtandao utakaowezesha kutoa misaada
ya kiufundi wa kijasiria mali na upatikanaji wa mitaji na mikopo nafuu kwa
vijana, ruzuku maalumu za kundeleza vikundi/asasi za vijana na tafiti
zinazolenga kukusanya taarifa zinazolenga kufuatilia uendeshaji na
mafanikio ya mradi na kuchangia katika kujenga mikakati na sera zitakozo
inua na kuendeleza ujasiria mali na ajira kwa vijana.
The Youth-to-Youth fund ni mfuko wa ruzuku maalumu inayotolewa kwa
vikundi/Asasi za vijana, ili kuendeleza stadi za vijana kuendesha asasi zao
na kujiendeleza katika ujasiria mali endelevu.
Lengo Kuu Lengo kuu la ruzuku hii ni kupatia Asasi za vijana katika nchi za
Afrika Mashariki uwezo wa kushiriki kikamilifu katika kuchangia
maendeleo ya nchi zao. Kwa kupitia mfuko huu vijana
watajengewa uwezo, kuandaa na kutekeleza miradi mbalimbali
inayolenga kujengea uwezo wa kiufundi ili kukuza ujasirimali
endelevu na kukuza ajira kwa wanachama na vijana wengine zaidi
kupitia ujasiria mali endelevu.
Katika miaka miwili ya kwanza ya utekelezaji wa mradi huu hapa
Tanzania, mfuko huu maalumu wa vijana utalenga kufanikisha
mambo makuu matatu i) kuimarisha, kukuza na kujengea uwezo
Asasi zilizopo za vijana ii) kusaidia na kutoa miongozo katika
kuanzisha na kukuza Asasi za vijana, iii) kusaidia kuanzishwa,
Kukuza na kuendeleza mitandao ya kijasiria mali ya vijana katika
wilaya mbalimalimbali hapa nchini.
www.ilo.org/yen 2
2. WALENGWA WA MFUKO HUU WA RUZUKU WA VIJANA TANZANIA?
WENYEVIGEZO Asasi zisizo za kiserikali za vijana na vikundi vya vijana
VYA KUSHIRIKI
“Asasi za Vijana” hizi ni asasi zilizosajiliwa na kutambulika kisheria
zilizo na wanachama na uongozi wa vijana wenye umri wa miaka 15-
35.
“Vikundi vya Vijana” hivi ni vikundi maalumu vya kujitolea
vinavyoundwa kwa hiari na vijana walio na umri wa miaka 15-35 ,
vikundi hivi vyaweza kuwa na wanachama waliojiunga kwa hiari kati
ya vijana 5 na kuendelea kwa mfano vikundi vya vijana walio
mashuleni.
Ikumbukwe kua vikundi au Asasi za vijana ni zile tu zinazoundwa na
vijana, vyenye wanachama na kuongozwa na vijana walio na umri
wa miaka 15-35.
Ili kushiriki katika mfuko huu wa vijana, andiko la mradi ni lazima liandikwe
na kuwasilishwa na vijana na kutekelezwa na vijana chini ya uongozi wa
kijana wa kike/kiume mwenye umri wa kati ya miaka 18-35.
Ruzuku hii haitatolewa kwa mtu au watu asasi au vikundi visivyosajiliwa
hivyo basi inashauriwa kwamba vikundi au asasi zisizo sajiliwa kisheria
kushirikia na asasi zilizosajiliwa kisheria na kuomba ruzuku.
Wilaya zikazoshiriki katika awamu hii ni pamoja na wilaya za Bagamoyo,
Handeni, Lindi Urban, Micheweni, Mtwara Rural, Mpanda, Musoma Urban,
Rufiji, Singida Urban, Tabora, Unguja North A, na Urambo tu.
Waombaji Kipaumbele kitatolewa kwa andiko la mradi litakalowasilishwa na Asasi
watakaopewa zifuatazo:
kipaumbele
- Asasi au vikundi vya vijana wa kike
- Asasi na vikundi vinavyoendeshwa na vijana
- Zitazowasilishwa na asasi/vikundi kwa kushirikiana wajasiriliamali
binafsi, asasi za kibiashara, mifuko na asasi za kiserikali.
Kipaumbele kitatolewa pia kwa maandiko ya miradi yanayolenga kuchangia
kukuza na kuendeleza ujasiria mali kwa vijana, ajira binafsi kwa vijana na
hasa vijana walio katika mazingira magumu na hatarishi.
www.ilo.org/yen 3
Muda wa mradi Miradi yote ya awamu hii ya kwanza itatekelezwa kwa muda usiozidi
mwaka mmoja yaani miezi 12 tokea ruzuku itakapotolewa, na itatakiwa
kutekelezwa na kumalizika kabla ya mwisho wa mwaka 2011.
Uchangiaji Kila Asasi itayopata ruzuku itawajibika kuchangia asilimia ( 25% ) ya ruzuku
itakayotolewa, michango hiyo yaweza kuwa ya kifedha au muda (utumishi
wa wafanyakazi)
Lugha Maandiko yote ya mradi ni lazima yawasilishwe kwa lugha ya KIINGEREZA,
tafsiri kwa Kiswahili inaweza kuwasilishwa kwa ufahamu tu. Andiko lolote
litakalowasilishwa kwa lugha ingine zaidi ya KIINGEREZA (ENGLISH)
haitabaliwa wala kushughulikiwa.
3. RUZUKU ITAKAYOTOLEWA
Ruzuku Kiasi cha ruzuku kitakachotolewa kwa wale watakaowasilisha andiko la
mradi la kibunifu na linaloshinda vigezo vilivyotolewa, ni fedha taslimu za
kitanzania zikiwa na thamani ya dola za kimarekani USD 5,000 - 20,000
pamoja na msaada wa kiufundi, mafunzo na kusaidia upatikanaji wa
mikopo nafuu na ruzuku toka mashirika ya kifedha. Mifuko hii ya ruzuku
itatolewa kwa kutegemea tathmini zitakazoelekeza aina ya ruzuku
itakayotolewa kwa asasi au kikundi. Mafunzo na misaada ya kiufundi
itaendelewa kutolewa katika muda wote wa kuandika na kuwasilisha
andiko la mradi.
Ikumbukwe kwamba katika kila awamu ya utoaji wa ruzuku ni Asasi au
vikundi 5 tu ndio vitapata ruzuku, pia asasi na vikundi 20-30 zaidi
vitapatiwa mafunzo ya kiufundi katika kujenga asasi zao na kuelekezwa
jinsi ya kupata ruzuku na mikopo toka mashirika mengine ya kifedha.
4. JINSI YA KUSHIRIKI
Jaza fomu maalumu zilizotolewa, kiufasaha na kikamilifu na kuzituma kwa
barua pepe zikiwa katika mfumo wa (PDF or Microsoft Word Document
attachment) tu katika anuani hii yefafrica@ilo.org kabla ya tarehe 31
Augusti, 2010. Andika kichwa cha barua: Tanzania Y2Yf, short proposal,
[jina la Asasi/kikundi].
5. MCHAKATO WA KUCHAGUA WASHIRIKI
MCHAKATO WA KUTATHMINI NA KUCHAGUA WASHINDI
Mchakato Mchakato wa kuchagua washindi utachukua hatua kuu 3 ambazo ni makini
na za wazi:
www.ilo.org/yen 4
Hatua ya kwanza I: Asasi/vikundi vya vijana vitaalikwa kujaza na kuwasilisha
fomu maalumu yaani “Short Proposals for Innovative Ideas”. Fomu
zitakazojazwa kikamilifu na kuwasilishwa kabla ya tarehe ya mwisho zita
fanyiwa tathmini na kamati itayaoundwa na wataalamu na wadau
mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi ili kuchagua maandiko (fomu)
zilizofikia viwango na vigezo vilivyoweka, washindi hao wa hatua ya
kwanza wataingia hatua ya pili yaani watakuwa “semi-finalists”.
Hatua ya II: Washindi wa hatua ya kwanza yaani “semi-finalists” watapewa
mafunzo maalumu ya kuandika andiko kuu la mradi na kusaidiwa katika
hatua zote za kuandika andiko hilo pamoja na kutengeneza plani ya
utekelezaji yaani “Full Proposal for the Implementation Plan”. Asasi
zitakazo andika na kuwasilisha maandiko ya kibunifu na yanayotekelezeka
watatembelewa na kamati maalumu ya tathmini kabla ya kuchaguliwa
kuingia hatua ya tatu yaani “finalists”.
Hatua ya III: Hatua hii ya tatu itahusisha kongamano la kuchagua washindi
na kujifunza toka kwa asasi zingine zilizoshiriki. Hatua hii itahusisha
wataalamu wajuu zaidi watakao fanya usahili wa hapo kwa hapo na
kuchagua washindi wasiopungua wa 5 watakaopewa ruzuku ya kuendesha
miradi kutokana na maandiko yao yaliyowasilishwa.
Washindi watachaguliwa kwa kutimia vigezo vya kiushindani, usawa na
uwazi wa hali ya juu. Ili kuhakikisha uwazi katika tathmini na uchaguzi kila
fomu na maandiko yote yatapewa namba za siri, hii itahusisha kuondoa
majina na anuani ya asasi/vikundi vya washiriki, tathmini pia itafanywa na
wadau mbali mbali wa nje na ndani na wenye utaalamu katika kufanya
tathmini za miradi na hasa miradi ya ujasiria mali.
Uchaguzi wa Hatua ya I (Fomu za Awali):
washindi:
Katika hatua ya kwanza uchaguzi utaaangalia zaidi andiko lenye ubunifu,
lenye uhakika wa kkuchangia suluhisho kwa matatizo yaliyo ainishwa na
uwezo wa kutekelezeka sehemu nyingine.
i) Ubunifu na uhakika katika kutatua matatizo yaliyo ainishwa:
- Kwa kiasi gani andiko hili la mradi linatofautiana na miradi
mingine iliyofanyika na inayoondela katika kuendeleza ujasiria
mali kwa vijana wa Tanzania?
- Ni kwa jinsi gani mradi huo unaleta ubunifu, teckinologia mpya,
kujenga mashirikiano katika sekta husika?
ii) Andiko lililo na nafasi na uhakika wa kutekelezeka katika jamii
husika na kwingineko:
- Je andiko hili la mradi litachangia kuongeza ajira kwa vijana?
www.ilo.org/yen 5
- Kuna sababu zozote za kimsingi za zilizopelekea kupendekeza
mfumo uliopendekeza kutekeleza mradi huu?
- Je andiko hili la mradi lina fikia matakwa ya walengwa?
iii) Uwezekano wa kuigwa na kutumika mahala pengine na watu
wengine
- Wazo hilo/mradi huo una nafasi ya kuigwa na kutekelezwa
mahala pengine na watu wengine?
- Mradi huo unaweza kufanyika na kufikia vijana wengi zaidi?
Hatua ya II (Andiko la Mradi na mpango kazi wa utekelezaji):
Katika raundi hii ya pili ya mchakato wa kuandika andiko la mradi, tathmini
na uchambuzi makini utafanyika kutambua maandiko yaliyo ya kibunifu na
yanayoweza kutekelezeka na kutekelezwa mahala pengine. Tathmini hii
itafanyika kwa kutumia vigezo vifuatavyo.
i) Uwezo wa kuutekeleza mradi
ii) Umiliki wa mradi na mashirikiano ya wanajamii
iii) ushirikiano wa vijana wa kike
iv) mashirikiano na asasi, mashirika na vikundi vingine
6. KALENDA YA MCHAKATO NA MATUKIO?
Tarehe ya mwisho wa kuwasilisha andiko la miradi 31.08.2010
Taarifa kwa washindi wa raundi
ya kwanza ya mchakazo wa uandishi wa mradi *Septemba 2010
Tarehe ya mwisho ya kuwasilisha : *Oktoba 2010
Taarifa kwa washindi: *Novemba 2010
Kongamano la washindi pamoja na mavunzo
ya awali *Novemba/Desemba 2010
Kusaini mikataba: *Desemba 2010
* Angalizo: Muda huu ni kimipango tu unaweza kubadilika kutoka na mchakato unavyoendelea
www.ilo.org/yen 6
7. MAELEZO ZAIDI
Mikataba ya Ruzuku Asasi zilizoshinda na kupatiwa ruzuku, zitaingia mkataba maalumu
utakaondaliwa na YEN kwa kufuata vigezo vya YEN, mikataba hiyo itaweka
wazi haki na matarajio ya YEN katika kutekeleza mradi. Hii ni pamoja
nayafutayo:
Malipo yatafanyika Asasi/vikundi kwa awamu mbili hadi tatu, mara
baada ya kuwasilisha repoti fasaha na kamili za fedha na utekelezaji
wa mradi.
YEN itakua na haki ya kuita wataalamu maalumu yaani (Auditors)
kufanya ukaguzi wa uendeshaji wa mradi.
Iwapo Asasi/kikundi kitashindwa kutekeleza mradi kama
ilivyokubaliana katika makataba, sekretariati ya YEN itakua na haki
ya kusimamisha malipo na kuvunja mkataba na kudai fidia ya
malipo kama ilivyo ilivyokubalika katika mkataba rasmi.
Pamoja na ruzuku itakayotolewa washindi watapatiwa msada wa kiufundi
ikiwa ni pamoja na kufanyiwa tathmini kutambua aina ya mafunzo
yatakayohitajika, kupatiwa mafunzo, kusaidia kujenga mtandao na
mashirikiano na wafanyabiashara, mashirika yatoayo mikopo na ruzuku
kwa maendeleo ya vijana, wataalamu mbalimbali watakao toa msaada wa
kiufundi katika kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa ustadi na ufasaha
zaidi. Ikumbukwe kwamba sehemu ya ruzuku itakayotolewa kwa asasi na
vikundi vitakavyoshonda katika mchakato huu zitatumika kulipia baadhi ya
mafunzo yatakayo hitajika.
Anuani kwa Kwa maelezo na maelekezo zaidi tafadhali wasiliana na Afisa Mradi –
ajili ya maelezo zaidi Tanzania kwa anuani zilizotolewa hapo chini.
National Youth-to-Youth Fund Coordinator
Jina: Noreen Toroka
Simu Ofisini: (022) 219 6727
Simu : (07) 874 32410
Baeua pepe: toroka@ilo.org
Kwa kutuma fomu: yefafrica@ilo.org
Tovuti: www.ilo.org/yen
www.ilo.org/yen 7
MAELEKEZO YA KUJAZA FOMU
Tafadhali zingatia kwamba:Hii siyo fomu rasmi lakini ni tafsiri tu. Tafadhali tumia fomu rasmi ya maombi
ambayo imetolewa kwa lugha ya Kiingereza.Maelezo haya ni ya kuwasaidia wale wanaohitaji kuelewa
namna ya kujaza, kwa ufasaha na kikamilifu.
Kabla ya kujaza fomu rasmi tafadhali isome kwa uangalifu na zingatia maelekezo yote yaliyotolewa, kisha
jibu maswali au vidokezo kwa uangalifu na ukamilifu. Inasisitizwa kwamba fomu isiyojazwa kwa usahihi
na ukamilifu haitashughulikiwa. Tafadhali usitume viambatanisho vyovyote hadi pale utakapoombwa
kuvituma.
Fomu ya maombi iliyojazwa kwa ukamilifu itumwe kwa barua pepe (e-mail) kwenda yefafrica@ilo.org
kabla ya tarehe 31-08-2010. ikiwa na kichwa cha habari: Tanzania Y2Yf, short proposal, [Jina la
kikundi/Asasi)
ANGALIZO
Maombi yatumwe kwa kutumia fomu rasmi iliyojazwa kwa mashine, yaani komputa (Microsoft Word
Document).Fomu iliyojazwa kwa mkono haitakubaliwa. Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana na ofisi kwa
anuani ifutayo:
National Youth-to-Youth Fund Coordinator
Jina: Noreen Toroka
Simu Ofisini: (022) 219 6727
Simu : (07) 874 32410
Baeua pepe: toroka@ilo.org
Kwa kutuma fomu: yefafrica@ilo.org
Tovuti: www.ilo.org/yen
www.ilo.org/yen 8
SEHEMU A: MAELEZO YA MUOMBAJI
Sehemu Hii Ijazwe Na Isizidi Kurasa 2
1. Maelezo/Anuani ya Asasi/Kikundi
Hapa unatakiwa ujaze maelezo kama ifuatavyo
o Jina la Asasi/Kikundi
o Jina wa meneja wa mradi
o Umri wa meneja wa mradi (18-35)
o Jinsia wa meneja wa mradi
o Wadhifa wake kwa sasa
o Namba yake ya Simu
o Anuani ya barua pepe (kama anayo)
o Anuani ya sanduku la barua na
o tovuti kama ipo
2. Aina ya Asasi
Katika kipengele hiki unatakiwa kutoa maelezo mafupi yanayohusu, Ikiwa ni pamoja na kuchagua jibu
sahihi kutokana na swali lililo ulizwa.
Asasi/Kikundi kama vile Asasi isiyo ya Kiserikali:
Asasi ya vijana iliyosajiliwa (Ndiyo/Hapana)… je inayoongozwa na vijana? (Ndiyo/Hapana)
Kikundi cha watu/vijana wasiopungua 5, (Ndiyo/Hapana)… je kinaoongozwa na vijana?
(Ndiyo/Hapana)
Tarehe ya kuanzishwa
Aina na namba ya usajili
Namba ya Usajili
3. Madhumuni na Aina ya Asasi/Kikundi
Kwa kifupi, unatakiwa utoe maelezo ya madhumuni, na malengo ya Asasi au kikundi chenu.
Eleza ni kitu gani kinachofanya Asasi au kikundi chenu kitambulike kama ni cha vijana?
Kama ni Asasi/kikundi cha vijana tafadhali eleza.
4. Wadau/mashirika wengine/mengine mnaoshirikiana /mnayoshirikiana nao/nayo
Katika sehemu hii ya nne unatakiwa kutaja asasi/ mashirika/wadau unaoshirikiana nao.
Je unamashirika/asasi unayoshirikiana nayo? (Ndiyo/Hapana)
Kama ndiyo, toa maelezo kama ifuatavyo. Kama kuna mashirika/Asasi au vikundi zaidi tafadhali
tumia kurasa nyingine moja kutoa maelezo yao kama iliulizwa.
o Jina la Asasi/Kikundi/Shirika.
o Jina la kiongozi au mhuika mkuu
o Wadhifa wa mhusika mkuu
o Simu
o Barua pepe
o Anuani zao za posta
o Tovuti (kama ipo)
www.ilo.org/yen 9
o Aina ya Asasi/kikukundi/shirika (tafadhali eleza1)
o Asasi/kikundi/shirika limesajiliwa (Ndiyo/Hapana)
o Kama ndiyo namba yao ya usajili
o Ushirikiano huo ulianza lini (mwezi, mwaka)
SEHEMU B: AINISHO LA MRADI
5. Jina la Mradi
Katika sehemu hii unatakiwa kujaza yafuatayo.
Jina la Mradi
6. Muda wa Mradi
Makadirio ya kipindi cha utekelezaji wa Mradi, yaani matarajio ya Mradi utaanza lini na
utamalizika au kukamilika lini. (zingatia kuwa ukomo wa utekelezaji wa Mradi ni miezi 12 tu).
7. Wilaya gani
Mradi huo unakusudiwa kutekelezwa katika wilaya gani kati ya wilaya zilizotajwa hapa chini?
8. Kiasi cha Fedha
Tafadhali eleza kiasi cha fedha zitakazohitajika kutekeleza mradi.
9. Walengwa
Katika sehemu hii unatakiwa kutoa maelezo kuhusu walengwa wa mradi wako.
Jee ni vijana wa namna gani unaowalenga?
o Vijana wa kike
o Vijana wa kiume
o Vijana waishio vijijini
o Vijana waishio mjini
o Vijana walio nje ya shule
o Vijana wenye familia
o Vijana wakimbizi
o Vijana walemavu
o Vijana wasio na elimu
o Walengwa wasio katika kundi maalumu la vijana
o Vijana wengine (toa maelezo)
1
Asasi za kijamii, Asasi zisizo za kiserikali, Mashirika ya kidini, Mashirika ya kiserikali, Mashirika ya kibinnafsi, mifuko ya kiserikali, ya kidini nay a
kibinafsi ya kimaendeleo, asasi na jumuia za kielimu, Asasi na mashirika ya kimataifa ya Maendeleo.
www.ilo.org/yen 10
SEHEMU C: MAELEZO YA KINA KUHUSU MRADI
Sehemu Hii Ijazwe Na Isizidi Kurasa 3
10. Ainisho la Tatizo:
a. Ni vijana gani unaotarajia kuwalenga?
b. Ni matatizo gani ya kiajira na/au ya kijasiriamali yanayowakabili vijana wa eneo lako?
c. Uliyajuaje/uliyatambuaje matatizo hayo?
d. Jee kuna umuhimu gani wa kuyatatua matatizo hayo?
11. Wazo jipya:
a. Jee ni wazo gani jipya ulilonalo kuhusu mradi huu?
b. Ni kwa njia gani wazo la mradi wako litatatua matatizo ya vijana unaowalenga?
c. Ni kwa jinsi gani mradi huu utasaidia kuongeza/kuendeleza ujasiriliamali endelevu kwa vijana?
12. Lengo la Mradi:
a. Katika sehemu hii unatakiwa kuainisha lengo kuu la mradi kwa kueleza ni kitu gani au malengo
gani yanatarajiwa kufikiwa na mradi huu?
b. Ni mafanikio gani yanatarajiwa na mradi huu ( tafadhali yataje na/au yaorodheshe).
13. Utekelezaji:
Katika sehemu hii unatakiwa kueleza hatua mbalimbali zizakazochukuliwa ili kufikia malengo na
matarajio ya mradi? Taja hatua kuu 5 kwa mpangilio fasaha.
14. Ubunifu:
Katika sehemu hii ya 14 unatakiwa kueleza ni kwa jinsi gani mradi wako ni wa kibunifu na una
tofauti gani na miradi mingine?
www.ilo.org/yen 11
SEHEMU D: UFUATILIAJI
15. Katika sehemu hii unaombwa kueleza namna ulivyopata taarifa kuhusu mpango wa Youth
to Youth Fund unaoratibiwa na YEF. Tafadhali weka alama X kwa majibu yako kama vile:
Maelezo maalumu kuhusu YEF
Tovuti
Majarida
Radio
Vipeperushi
Marafiki
Wadau wengine (Eleza):
www.ilo.org/yen 12
Get documents about "